NYOTA +255757570194
UNAJIMU AU ASTROLOJIA NI ELIMU JUU YA UHUSIANO KATI YA NYOTA NA MAISHA YA
BINADAMU DUNIANI. WANAZUONI WA UNAJIMU WANAELEZA YA KWAMBA NYOTA ZINAATHIRI
MAISHA YA WATU NA MATUKIO KAMA AMANI, VITA AU MAAFA. MAHUSIANO HAYA HAYAJAWEZA
KUTHIBITISHWA NA SAYANSI YA FIZIKIA AU SAYANSI NYINGINE. ALAMA ZA NYOTA 12 NI
MSINGI WA FALSAFA HII YA UNAJIMU.
ASTROLOGIA IMEKUWA IKITUMIKA KWA MIAKA MINGI LAKINI SIKU ZOTE IMEKUWA
IKIPATA UPINZANI MKUBWA TOKA KWA WANA SAYANSI.
ASTROLOJIA INA MISINGI TOKEA ENZI ZA ZAMANI WAKATI SAYANSI ILIPOKUWA YA
CHINI NA IMANI ZA KIROHO NA KIUNGU ZIKIWA ZA KIWANGO CHA JUU KATIKA JAMII
NYINGI.
BAADHI YA TAFITI ZILIZOFANYWA KUCHUNGUZA USAHIHI WA ASTROLOJIA UNAONYESHA
KUNA USAHIHI WA ASILIMIA KAMA 3O TU. HII SI HABA,KUNA UKWELI BASI KATIKA HILI
JAPO BADO KUNA UPINZANI MKUBWA TOKA KATIKA ULIMWENGU WA SAYANSI YA KISASA.
[SOMA PIA:MADHARA YA MWEZI KATIKA HISIA NA TABIA ZA BINADAMU:KUNA UKWELI? ,
NYOTA NA KAZI ZENYE MAFANIKIO ]
TABIA ZA WATU NA ALAMA ZA NYOTA
ALAMA ZA NYOTA ZINABASHIRI TABIA NA HAIBA YA BINADAMU KATIKA DUNIA.
MPANGILIO AU NAFASI YA SAYARI KATIKA MZUNGUKO WAKE ANGANI UNAAMINIKA KULETA
ATHARI KWA BINADAMU NA MATUKIO KATIKA DUNIA.
KUNA ALAMA 12 ZA KIASTROLOJIA. KILA MOJA INA MVUTO WA NGUVU WA KIPEKEE TOKA KATIKA
NYOTA.
ALAMA HIZI NI KAMA IFUATAVYO:
SAMAKI (PISCES):FEB 19 – MACHI 20
KONDOO (ARIES): MACHI 21 – APRILI 19
NG’OMBE (TAURUS): APRILI 20 – MEI 21
MAPACHA:(GEMINI ): MEI 22 – JUNI 20
KAA(CANCER): JUNI 21 – JULAI 22
SIMBA(LEO): JULAI 23 – AGOSTI 22
MASHUKE(VIRGO):AGOSTI 23 – SEPT 22
MIZANI (LIBRA): SEPT 23 – OKT 22
NG’E (SCORPIO): OKT 24- NOV 21
MSHALE (SAGITTARIUS): NOV 22- DES 21
MBUZI(CAPRICORN):DES 22 – JAN 19
NDOO (AQUARIUS):JAN 20 – FEB 18
MAKUNDI YA ALAMA ZA NYOTA:
ALAMA HIZI 12 ZA NYOTA ZINAGAWANYIKA KATIKA ELEMENTI 4 ZIJULIKANAZO KAMA:
MOTO:YENYE MATAMANIO YA MAFANIKIO AU MAKUU,DADISI
MAJI:YENYE KUBADILIKA NA YENYE UWEZO WA UFAHAMU WA NDANI
HEWA:IMARA NA YENYE KUKUZA AU KUENDELEZA
UDONGO:YENYE ELIMU AU UWEZO WA KUTAMBUA NA YENYE KUHAMASISHA
HIZI NI ELEMENTI NNE ZINAZOONGOZA ASTROLOGIA. KILA KIMOJAWAPO KINABEBA TABIA
FULANI.
ALAMA HIZI 12 ZA NYOTA ZIMEGAWANYIKA KAMA IFUATAVYO:
MOTO: KONDOO, SIMBA,MSHALE
MAJI: NG’E, SAMAKI, KAA
HEWA: MAPACHA, MIZANI, NDOO
UDONGO: NG’OMBE,MASHUKE,MBUZI
KILA ALAMA YA NYOTA 12 ZIMEGAWANYIKA PIA KATIKA MAKUNDI MENGINE MATATU
AMBAYO NI:
YENYE UMUHIMU AU MSINGI “CARDINAL”: KONDOO, KAA,MIZANI,MBUZI
YENYE KUBADILIKA “MUTABLE”: NG’OMBE, SIMBA, NG’E NA NDOO
ISIYOBADILIKA “FIXED”: MAPACHA, MIZANI, MSHALE NA SAMAKI
ALAMA AMBAYO IKO KATIKA MOTO NA IKO KATIKA KUNDI LA MSINGI HUWA NA
TABIA ZA UPINZANI NA UBISHANI WA HALI YA JUU KAMA KONDOO
ALAMA AMBAYO IPO KATIKA KUNDI LA UDONGO NA KUBADILIKA HUWA NA TABIA ZA
UTULIVU WA HALI YA JUU KAMA NG’OMBE.
HAIBA NA TABIA ZA ALAMA ZA NYOTA
#1 NYOTA YA KONDOO: MACHI 21 – APRILI 19
ALAMA-ZA-NYOTA_KONDOO
NI MWENYE MAAMUZI YASIYOPINDA NA MTENDAJI MZURI WA KAZI.
ANATEGEMEA MAKUU JUU YAKE MWENYEWE NA KUTOKA KWA WENGINE
MWENYE KUJITEGEMEA NA MWENYE ARI YA HALI YA JUU
ANAUTHUBUTU WA KUJARIBU MAMBO MAKUBWA
MWENZILISHI WA MAMBO NA MBUNIFU
KIONGOZI
MUONGEAJI
NI MWENYE HISIA KALI NA ASIYE NA UVUMILIVU MKUBWA.
MWAMINIFU KWA MARAFIKI NA FAMILIA
ANAJALI MPENZI WAKE NA MWENYE HISIA KALI ZA MAPENZI
#2
NYOTA YA NG’OMBE: APRILI 20 -MEI 20
ALAMA-ZA-NYOTA_NGOMBE
NI ALAMA YA UDONGO:
NI MWENYE NGUVU NA MSTAHIMILIVU KIMWILI NA KIAKILI
MAKINI NA MUANGALIFU
ANA KIBURI NA ASIYEKUBALI KUSHINDWA KIRAHISI
MSTAHIMILIVU
MWENYE KUTEGEMEWA
NI MGUMU KUBADILIKA
ANAPENDA VITU VIZURI NA VYA THAMANI
UNAPENDA UREMBO NA VITU VYA KUPENDEZA
MWENYE HISIA ZILIZOFICHIKA
HUENDA AKAONEKANA MBINAFSI LAKINI NI WENYE KUTOA WAKIWA NA
MALI AU FEDHA.
#3 NYOTA YA MAPACHA: MEI 21 – JUNI 20
ALAMA-ZA-NYOTA_MAPACHA
NI ALAMA YA HEWA:
NI MWENYE KIPAJI KIKUBWA,MWENYE KUBADILIKA NA ANAYECHOKA
HARAKA NA KUKATA TAMAA
ANAFIKIRI KWA HARAKA NA MCHESHI
NI MWASILIANAJI MZURI
NI MTU ANAYEPENDA WATU NA MWENYE KUPENDA MABADILIKO.
MWENYE KUAMUA KWA AKILI NA MBUNIFU
HANA UTULIVU
ANA MIPANGO NA MALENGO MAKUBWA
MWENYE KUBADILIKA KIRAHISI
#4 NYOTA YA KAA: JUNI 21 – JULAI 22
ALAMA-ZA-NYOTA_KAA
NI ALAMA YA MAJI:
ANAPENDA KUKAA NYUMBANI NA KUWA NA MAKAZI MAZURI YENYE
KUMPAUTULIVU ,USALAMA NA AMANI
ANAPENDA MARAFIKI NA FAMILIA. ANANPENDA KUFUATILIA HISTORIA YA
UKOO
HISIA ZAKE NI ZA WAZI NA NI RAHISI KUJULIKANA
ANA HURUMA
NI MWANGALIFU
MKIMYA NA
#5 NYOTA YA SIMBA: JULAI 23 – AGOSTI 22
ALAMA-ZA-NYOTA_SIMBA
NI ALAMA YA MOTO:
KAMA ALIVYO SIMBA NI JASIRI NA MWENYE UTHUBUTU.
ANAPENDA KUONEKANA NA WATU
SANAA NI MOJAWAPO YA MAENEO AMBAYO ANAYAMUDU NA AMBAYO
YANAMFANYA AFANIKIWE
WANA MAAMUZI MAZURI NA NI WAIGIZAJI MAHIRI.
NI WENYE MOYO WA KUTOA NA WENYE UPENDO MKUBWA
NI VIONGOZI WAZURI NA WENYE NGUVU
MWENYE MATUMAINI MAZURI
MWENYE KUHESHIMIKA
MSHINDANI
MPANGILIAJI MZURI WA MAMBO YA KUFANYA
MWENYE MVUTO
#6 NYOTA YA MASHUKE: AGOSTI 23 – SEPTEMBA 22
ALAMA-ZA-NYOTA_MASHUKE
NI NYOTA YENYE ALAMA YA UDONGO
ANA MATEGEMEO MAKUBWA JUU YAKE MWENYEWE NA KUTOKA KWA WATU
WENGINE
NI MWENYE UJUZI NA MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA KAZINI
NI MCHUNGUZI NA MDADISI WA MAMBO NA MWENYE KUFANYA KITU KIMOJA
KWA WAKATI MMOJA.
WAPANGILI WAZURI WA MUDA NA WATEKELEZAJI
NI MDADISI NA MBISHI KATIKA KUHAKIKISHA MAMBO YANAFANYIKA KWA
UKAMILIFU.
NI WAFANYA KAZI WENYE UMAKINI NA NI WAANGALIFU KATIKA KAZI
ZAO.
WANAJALI AFYA
#7 NYOTA YA MIZANI: SEPTEMBA 23 – OKTOBA 22
ALAMA-ZA-NYOTA_MIZANI
NI ALAMA YA HEWA. MWENYE NYOTA YA MIZANI ANATUMIA MUDA MWINGI KATIKA KULETA
USAWA NA HAKI NA KUSURUHISHA MIGOGORO.
MIZANI ANATUMIA AKILI ZAIDI KULIKO NGUVU ZA MWILI.
HUSIMAMIA HAKI NA USAWA
ANAPENDA SANAA NA UREMBO
WABUNIFU WA SANAA
NI MPENZI WA MUZIKI
NI MUWAZI KATIKA KUONYESHA UPENDO
ANA USTADI WA KUKABILIANA NA MAMBO YA KIJAMII
ANATOA MATAZAMO WAKE PALE TU ANAPOCHOKOZWA AU ANAPOGUSWA
KIHISIA
MPENDA AMANI
WENYE MVUTO WA KUPENDWA
#8 NYOTA YA NG’E: OKTOBA 23 – NOVEMBA 21
ALAMA-ZA-NYOTA_NGE
NI ALAMA YA NYOTA YA MAJI NA NI MWENYE HISIA NZITO
ANAPENDA MAMBO MAKUBWA NA MAISHA YA MAZURI
MJASIRIAMALI NAMWENYE UWEZO WA KUKABILIANA NA VIZINGITI
VIKUBWA
ANAPENDA MALUMBANO MAKALI
WANATUMIA NGUVU
JASIRI
WASTAHIMILIVU
WASHINDANI
WANAUWEZO ,
WACHUNGUZI WA MAMBO
WASIRI
NI MPENZI MZURI NA MWENYE TABIA ZA UMILIKI
WANAJITEGEMEA
NI WENYE MAAMUZI
#9 NYOTA YA MSHALE: NOVEMBA 22 – DESEMBA 21
ALAMA-ZA-NYOTA_MSHALE
NI ALAMA YA MOTO NA NI MWENYE MAPENZI MAZITO NA VITU
MWANAFALSAFA NA MKUSANYAJI WA HABARI
MWENYE UWEZO MKUBWA KIAKILI MA ANAPENDA CHANGAMOTO
NI MWENYE NGUVU AMBAZO HUMFANYA MARA ZOTE AENDE MBELE.
NI MWENYE KUPENDA UHURU
NI MPENZI MWENYE MVUTO NA ANAPENDA KUMRIDHISHA MPENZI WAKE
RAFIKI
MWENYE ARI
HAWANA UTULIVU
WAAMINIFU NA WAKWELI
WANAPENDA SAFARI
#10 NYOTA YA MBUZI: DESEMBA 22 – JANUARI 19
ALAMA-ZA-NYOTA_MBUZI
NI ALAMA YA UDONGO NA MWENYE KUHITAJI NYUMBA YENYE AMANI ILI KUHISI
UKAMILIFU.
MWENYE MALENGO , MIPANGO NA MATARAJIO MAKUBWA
NI MTATUAJI WA MATATIZO KWA VITENDO NA MAPANGILIAJI MZURI WA
MAMBO-MTENDAJI
NI MWENYE MIPANGO NA MFUATILIAJI WA MIPANGO YAKE
SI MSHIRIKISHAJI MZURI MPAKA AOMBWE AU ASUKUMWE.
NI MPENZI MZURI NA RAFIKI WA MAISHA
MGUMU KUBADILIKA
MBISHI NA ASIYEKUBARI KUSHINDWA KIRAHISI
MFANYABIASHARA
MWAJIBIKAJI
#11 NYOTA YA NDOO: JANUARI 20 – FEBRUARI 18
ALAMA-ZA-NYOTA_NDOO
NI ALAMA YA HEWA:
NI MBINAFSI NA ASIYEPENDA KUFUATA UTARATIBU AU SHERIA.
WAKIPEKEE
ANAEJITEGEMEA NA HUPENDA KUWA PEKE YAKE
MWENYE HURUMA
MUONA MBALI
MWENYE UFAHAMU WA HALI YA JUU NMA MBUNIFU
ANAFANYA MARAFIKI WA AINA MBALIMBALI
ANA UTU NA MWENYE KUDAI HAKI
ANAPENDWA NA WATU NA ANATEGENEZA URAFIKI KWA HARAKA
ANAPENDA SANAA NA MAISHA YA ANASA.
#12 NYOTA YA SAMAKI: FEBRUARI 19 – MACHI 20
ALAMA-ZA-NYOTA_SAMAKI
NI ALAMA YA MAJI NA NI MWENYE UFAHAMU WA HALI YA JUU WA MAMBO.
NI MKWELI NA MWENYE HISIA NZITO
HANA UBINAFSI
NI MPENZI MWAMINIFU NA RAFIKI
MPENDA AMANI
ANA HURUMA
ANAJITOA
WANA NDOTO
WABUNIFU
WANA AIBU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MJUE JINI MAHABA: Fahamu Mengi kuhusu jini mahaba +255757570194
MJUE JINI MAHABA: Fahamu Mengi kuhusu jini mahaba Habari wakuu! Wengi miongoni mwenu huona kila ninapotoa thread huona kama vile huf...
-
FAHAMU KUHUSU MMEA WA MUOSHA FEDHA Muosha fedha unaingia kwenye orodha ya mimea saba ambayo inafanya kazi kubwa katika hitaji binaadam. Mt...
-
Juni 16, 2018 DAWA YA MWIZI AU MTU ALIYEKUZULUMU HII ni kwa wale walioibiwa jinsi ya kurudisha ktu chako na kuadhibu mwizi haraka m...
-
DALILI CHACHE 20 ZA MTU ALIEKUMBWA NA JINI Zifuatazo ni baadhi tu ya dalili za mtu anayekubwa na jini wa kutumwa au wa kupamia: ...
No comments:
Post a Comment